Jeshi la Polisi Mkoani Arusha, limemkamata Isaack Habakuk Emily, kwa kosa la kumtukana Rais John Magufuli kuwa ni bwege na kwamba hawezi fananishwa na Nyerere na kusambaza ujumbe kwenye mitandao ya kijamii.
Akizungumza ofisini kwake, leo jijini Arusha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa Machi 22 mwaka huu eneo la Hotel ya Anex jijini humo.
Amesema kuwa baada ya kumkamata alifanyiwa upekuzi na kukutwa na simu ya kiganjani aina ya Tecno iliyotumika kutenda kosa la kutuma ujumbe wa kumkashifu Dkt. Magufuli.
Mkumbo amesema kuwa mtuhumiwa huyo alituma ujumbe wa kashfa kwenye Facebook usemao:- “Mnamlinganishaje Magufuli na Nyerere,” na kutuma kwa watu mbalimbali kupitia simu yake ya mkononi.
Mkumbo amesema mtuhumiwa baada ya kusikia hivyo aliandika tena ujumbe kwenye mtandao wake usemao, “Hizi ni siasa za maigizo halafu mnamfananisha huyu bwege na Nyerere wapi Bwana,” amesema.
Amesema baada ya kutuma ujumbe huo uliwaudhi watu wengi waliopokea ujumbe huo na kuwakwaza, hali iliyosababisha kupeleka malalamiko yao Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mamlaka hiyo ilitoa taarifa polisi na hatua za kisheria zilianza kuchukuliwa.
Aidha amesema baada ya hapo walifanikiwa kumpata mtuhumiwa wa uhalifu kwa njia ya mtandao, kumtia hatiani na jana alifikishwa mahakamani kujibu shitaka lake.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa kutembelea Website hii coz
ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea kusoma na kufungua
LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website hii bila kusahau
kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
Whatsapp
+255 652 989 873
Karibu
sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA


No comments: