Wanadamu wote tumeumbwa na kupewa akili ambayo inabidi tuitumie vizuri ili kuweza kuishi vyema katika ulimwengu huu. kinachoshangaza ni kwamba wapo watu wachache tu ambao wamekuwa wakitumia akili vizuri na kufanya vitu vikubwa vinavyo wapatia mafanikio makubwa, huku wengi wetu tukiwa tumebaki kusema kuwa wao wamebahatika.
Hakuna watu waliozaliwa na bahati au mikosi, Wanadamu wote wanauwezo wakutumia akili vizuri na kujipatia kipato kikubwa sana. yapo mambo kadha wa kadha ambayo inabidi tuweze kuyafanya ili kuhakikisha kuwa tunasonga mbele na kuwa na maisha mazuri.
1. lazima mtu uwe na nidhamu katika kila kitu ambacho unakifanya.
Nidhamu inachukua sehemu kubwa sana kuliko unavyoweza kufikiria. hakikisha unakuwa na ratiba inayoeleweka ambayo itakuwa inakuongoza katika shughuli zako za kila siku. hii itaongeza ufanisi, lakini pia nidhamu humfanya mtu aheshimike na kuoneka ana thamani katika jamii, kitu kinachoweza kufanya watu wakupatie kazi mbalimbali kwakuwa wanaamini hauta waaibisha.
2. Uwe mwaminifu katika maisha yako.
Uaminifu umekuwa adimu sana kwa watu wengi, jambo linalopelekea watu kukosa nafasi mbalimbali kwakuhofiwa kufanya ubadhilifu. ukiwa mwaminifu ni rahisi kupata fursa nyingi na kazi nzuri zenye maslahi mazuri. uaminifu ni silaha kubawa sana katika maisha.watu waliofanikiwa walikuwa waaminifu kwa sehemu kubwa, hawakuwa na tamaa ndogondogo zisizo nafaida. hakuna haja ya kuiba fedha kidogo ambazo zitachafua jina lako na kufanya heshima yako ipotee. kumbuka kuwa ni rahisi sana kupoteza heshima kuliko kuijenga.
3. Usiwe na matumizi yasiyo na msingi.
Watu wengi hawafanikiwi kwasababu wanatamani maisha ya wenzao, wanapenda waonekane wana maisha ya juu wakati sio kweli. hakuna haja ya kutafuta sifa mbele za watu wakati ukirudi kwako unaanza kujuta kwa matumizi uliyoyafanya. weka akiba kwa kile unachokipata, achana na starehe zisizo za msingi. unywaji wa pombe unafilisi sana na unakwamisha sana maendeleo ya watu wengi. ishi maisha yaliyo ndani ya uwezo wako, ukiwaza kupiga hatua na si kudumaa hapohapo ulipo.
4. Fanya kazi kwa bidii na kwa malengo ili uwe na maisha mazuri.
Uvivu wa kufikiri na wa kufanya kazi unakwamisha maendeleo. tazama watu wote waliofanikiwa wanafanya sana kazi kwa bidii. Mwenyezi Mungu alisema kuwa asiyefanya kazi na asile, usichague kazi ya kufanya ilimradi isiwe inavunja sheria. tuache ubishoo wakuona kuwa kuna kazi ambazo hazikustahili wakati huna kazi ya kufanya.
5. Kuwa mbunifu.
Lakini pia tumia kipaji chako kujipatia kipato. usijilinganishe maisha yako na yawatu wengine, usiangalie watu waliofanikiwa bali angalia watu walio chini yako. mshukuru Mungu kwa uhai na uzima ulio nao. Fanya kazi kwa bidii ukimtanguliza Mungu utafanikiwa tu.
KWA HABARI ZAIDI
KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: