CHAMA cha Wasafirishaji wa Nyara Tanzania (TWEA) Kanda ya Kaskazini kimeiomba serikali kufanya uchunguzi wa kina na kuwaachia wanachama wao waliokamatwa mwishoni mwa wiki kwa tuhuma za kusafirisha tumbili hai 62 bila vibali huku wakieleza kuwa wapo tumbili wengine katika mabanda yao.
Miongoni mwa waliokamatwa ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Arusha Bird Traders na raia wawili wa Uholanzi waliokamatwa mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wakituhumiwa kusafirisha tumbili hao.
Akizungumza na waandishi wa habari , Mwenyekiti wa Twea Kanda ya Kaskazini, Othman Bhoki alisema kukamatwa kwa raia hao wawili KIA ambao ni Arten Vardanian (52) na Edward Vardanian (46) pamoja na Idd Misanya ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni iliyotumika kukamata tumbili hao ya Arusha Bird Traders ni kuwarudisha nyuma wafanyabiashara ambao wana vibali halali vya kuvuna tumbili hao.
Alisema wasafirishaji wa tumbili hao ambao ni Kampuni ya Arusha Bird Traders wana vibali halali vya kufanya biashara hiyo kwa maelekezo ya tangazo la Wizara ya Maliasili na Utalii.
Alisema suala hilo ni vyema likachunguzwa kwa kina kwani kampuni hiyo imewasilisha kibali halali cha kusafirisha wanyama hao chenye namba 29655 (Cites) kilichotolewa Februari 24, mwaka huu ambacho kinamalizika muda wake Agosti 23, mwaka huu.
Alisema kibali hicho kimeruhusu tumbili 62 kusafirishwa kwenda nchini Armenia na kukamatwa kwao kunaleta mkanganyiko kwani kwa mujibu wa kibali cha kukamata wanyama hao, kinaonesha kuruhusu daraja namba 13 la kuruhusu gawiwo la tumbili kuuzwa nje ya nchi.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
Karibu sana
LINK
CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: