Maambukizi ya UKIMWI yameanza kuongezeka tena kwa kasi mkoani Arusha huku waathirika wakubwa wakiwa ni kundi la watoto wanaoishi katika mazingira magumu,na wanaotoka katika familia maskini.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru Dk.Omary Chande amesema hali hiyo inachangiwa na kuanza kupungua kwa kasi ya kuhamasisha jamii kuepuka janga hilo kwa kuamini kuwa kwa sasa halipo wakati bado lipo na madhara yake ni makubwa.
Mkurugenzi wa Shirika la World Education linalosaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu Kanda ya Kaskazini kupitia mradi wake wa Pamoja Tuwalee Bi Lilian Badi amesema kasi ya upimaji wa UKIMWI katika jamii imepungua kwa kiasi kikubwa na tatizo ni kubwa zaidi kwa watoto wakiwemo wanaioshi katika mazingira magumu na wanaotoka katika familia.
Akizungumza na watoa huduma za UKIMWI wa kujitolea zaidi ya 200 wanaopatiwa mafunzo ya kusaidia janga hilo yanayotolewa na Taasisi za Pamoja Tuwalee na (CHSSC) zinazofadhiliwa na shirika la Misaada ya Marekani (USAID) Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daud Ntabenda amewataka watendaji kufufua upya kampeni za kukabiliana na UKIMWI.
LINK CLASSIC: Asante
sana kwa kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki
sana pia endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi
ndani ya Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako
kutembelea website hii
Pia waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
Whatsapp +255 652 989 873
Karibu sana
LINK
CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: