Afrika ni bara ambalo tafiti kadhaa zinafanyika na zimeendelea kufanyika, Matokeo ya Utafiti wa Africa Wealth umeitaja Zimbabwe kuwa ndio nchi Maskini. Inatajwa kuwa wizi wa kura, ukosefu wa kuheshimu haki za umiliki, vurugu, kukosekana kwa uhuru wa Habari, ni baadhi ya sababu ya Taifa hilo kuanguka na kuwa la mwisho.
Ripoti ya tatu ya mwaka ya Africa Wealth inasema watu wanaoishi Zimbabwe ni maskini katika bara la Afrika kwa kuwa na wastani wa pato la mtu mmojammoja ni US dola 200 ambapo ni kiasi ambacho watumishi wa umma wanakipata.
Ripoti imeeleza kuwa >>>’haki za umiliki ni muhimu kwa kuwezesha kujenga utajiri, Nchini Zimbabwe wamiliki wa Biashara hawana uhakika kama biashara zao au mali zao bado ni zao, hii inajenga hali ya woga kwa yeyote kutojitokeza kuwekeza kwenye nchi hiyo‘
Wakati Zimbabwe ikianguka na kuwa nchi maskini, kisiwa cha Maurtius kimepanda na kuonekana kuwa watu wake ni matajiri kwa hadi pato la US dola 21700 kwa utajiri wa mtu mmojammoja. Mafanikio ya Mauritius yamehusishwa na kupata haki za umiliki ambapo imeshuhudiwa watu matajiri wakihamia huko katika muongo uliopita.
Utafiti uliofanyika kwenye nchi 20, zote zimekuwa na ongezeko la pato kwa kipindi cha mwaka 2000 na 2015, kasoro Zimbabwe
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
Karibu sana
LINK
CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA


No comments: