sponsor

Slider

EMBROIDERY, DTF, & SCREEN PRINTING - T-shirt, Overall, Shirt , Pylon, Kofia Nk..


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » SERIKALI KUJENGA NYUMBA ZA WAATHIRIKA WA MVUA YA MAWE


MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela amewataka wakazi wa kata ya Mwakata, wilayani Kahama ambao waliahidiwa kujengewa nyumba na serikali baada ya kuathiriwa na mvua ya mawe kuvuta subira wakati serikali iliyopo madarakani ikitekeleza ahadi iliyotolewa.

Serikali ya awamu ya nne iliahidi kujenga nyumba 342 za walioathirika na mvua ya mawe iliyosababisha zaidi ya watu 48 kupoteza maisha.

Akizungumza na wakazi wa Kata ya Mwakata siku tatu baada ya kuripoti katika kituo kipya cha kazi, Kilango alisema kuwa ucheleweshwaji wa ujenzi ulitokana na Serikali kuelekeza nguvu kufanikisha uchaguzi mkuu uliopita.

Mkuu huyo Mpya wa Mkoa wa Shinyanga alisema kuwa kutokana na uchaguzi huo kuisha kwa sasa Serikali itahakikisha kuwa hakuna mkazi yeyote wa kata ya Mwakata atakayeendelea kuishi kwa jirani.

“Kwa sasa uchaguzi umepita na tuiachie Serikali ifanye kazi yake ya ujenzi wa nyumba hizo na mimi ninawaahidi kuwa nitasimamia ujenzi huo, kwani maafa kama haya yalishawahi kutokea katika jimbo langu za Same enzi za ubunge wangu na Serikali ilichukua muda wa miaka miwili kutatua tatizo kama hilo”, alisema Kilango.


LINK CLASSIC: Asante sana kwa kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website hii
Pia waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini

INSTAGRAM           FACEBOOK    GOOGLE+

PINTEREST   TWITTER    LINKEDIN     DRIBBBLE

Karibu sana


LINK CLASSIC





 

 

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply