Msanii wa muziki wa R&B wa Tanzania, Rama Dee amesema kilichomfanya ahamie nchini Australia kwa mke wake ni mapenzi na sio kitu kingine.
Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Ijumaa hii, Rama Dee amedai anampenda mke wake ndiyo maana akahamua kumfuata Australia.
“Unajua ni mapenzi ndio yalinifanya kuhamia nchini Australia na hakuna kingine, yaani kifupi nimeolewa kule maana kwa mira zetu sisi watanzania huku mwanamke ndiyo huwa anamfuata mwanaume nyumbani kwake sasa kama mimi nimemfuata mwanamke kwao ina maana nimeolewa kule” alisema Rama Dee.
Katika hatua nyingine Rama Dee, amesema kuwa yeye hana tofauti yoyote na Mbunge wa Mbeya mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Joseph Mbilinyi alimaarufu kama Mr 2.
“Unajua watu wanasema mengi lakini mimi na Sugu tuko poa hata jana nilikuwa nakunywa soda na yeye sehemu fulani hivi” alisema Rama Dee
Sugu na Rama Dee walidaiwa kutofautiana kutokana na harakati za vinega.
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: