sponsor

Slider

EMBROIDERY, DTF, & SCREEN PRINTING - T-shirt, Overall, Shirt , Pylon, Kofia Nk..


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » POLISI WAFYATUA MABOMU YA MACHOZI MBELE YA BENKI YA CRDB, TAWI LA MBAGALA-RANGI TATU, NI KUFUATIA UBISHI WA WATEJA KUTUMIASIMU NDANI YA BENKI


POLISI wamelazimika kufyatua mabomu ya machozi kuwatawanya watu waliojikusanya mbele

ya Benki ya CRDB tawi la Mbagala-Rangi Tatu, baada ya mtu mmoja aliyekuwa akiongea na simu ndani ya benki hiyo kukaidi maagizo ya polisi ya kuacha kufanya hivyo mapema leo mchana Machi 11, 2016.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, watu watatu mmoja akiongea na simu na wengine wawili waki-chat, ndani ya benki hiyo, waliagizwa na mlinzi wa benki kuacha kufanya hivyo lakini wakakaidi.
Baada ya mlinzi kuona hivyo alitoa taarifa kituo cha polisi Mbagala-Maturubai, na ndipo polisi wakiwa ndani ya gari lao maarufu kama Defender, waliwasili kwenye eneo hilo na kuamuru watu hao ambao wanaelezwa kuwa wateja, kutoka ndani ya benki hiyo.
Hata hivyo palitokea mabishano baada ya mmoja wao kukaidi amri ya polisi na kuanza
kupigana nao.
Kuona hivyo watu walianza kujaa na polisi bila kufanya ajizi wakafyatua mabomu ya machozi kutawanya watu na kuwadhibiti “wateja’hao wabishi na hatimaye kufanikiwa kuondoka nao.
Hali hiyo ilizua tafrani hadi watu wakadhani kuwa palikuwepo na tukio la ujambazi kwani ni mwezi uliopita umbali wa mita chache kutoka kwenye benki hiyo, palitokea tukio baya la uvamizi wa benki ya Access ambapo watu kadhaa waliauawa wakiwemo polisi.

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply