Serikali ya Guinea Conakry imeanzisha elimu maalum kwa raia inayohusu namna ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Ebola,ambao umerejea tena nchini humo ambapo mpaka sasa watu watano wameshafariki dunia na wagonjwa kadhaa wamelazwa mahospitalini ikiwa ni miezi michache tu baada ya nchi hiyo kutangaza kuutokomeza ugonjwa huo hatari.
Kuzuka kwa ugonjwa huo tena nchini humo kumesababisha biashara katika soko kuu la mji mkuu liitwalo Madina kudorora mauzo yake ambapo wafanyabiashara wanasema hali ikiendelea hivyo kuna hatari wakashindwa kumudu maisha kwani awali walikuwa kila siku wanaondoka na faida kubwa.
Mratibu wa ugonjwa huo kitaifa,Fode Tass Silla amekiri kufanyika kwa uzembe katika kufuatilia na kuangalia namna watu wanavyosafiri kwenda nje ya nchi na wageni wanaokuja hali iliyosababisha kurejea tena kwa ugonjwa huo nchni humo.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
Karibu sana
LINK
CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: