Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohmaed Shein anatarajiwa kuzindua Baraza jipya la Wawakilishi Machi 30 ikiwa ni hatua za kuelekea kuanza kazi za Serikali baada ya kumalizika uchaguzi mkuu.
Akizungumza na wandishi wa habari Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Yahaya Khamis Hamad amesema kwamujibu wa Katiba na taratibu za kuendesha Baraza la Wawakilishi Rais wa Zanzibar ndiye mweye mamlaka ya kuitisha kikao hicho ambapo pia amesema watakitumia kuwaapisha Wajumbe wa Baraza na kuteua Wajumbe watano watakaowakilisha Baraza ndani ya Bunge.
Mapema Mtendaji huyo wa Baraza alimkabidhi fomu ya kugombea uspika kwa mgombea wa CCM Zubeir Ali Maulid huku akithibitisha kuwa ni mgombea pekee aliyejitokeza kuwania nafasi hiyo,ambapo akiongea na waandishi mgombea Uspika ambaye ni wa CCM na ana uhakika wa kupata kiti hicho amesisitiza ahadi zake kuwa Baraza pamoja kuwa ni la CCM halitoyumba na litakuwa na meno.
Baraza hilo la Wawakilishi limekamilika baada ya Uchaguzi Mkuu ambapo Majimbo 54 yamechukuliwa na CCM na viti 22 ni viti maalum vya wanawake huku Mjumbe mwingine na Mwanasheria Mkuu Wazanzibar huku kukiwa kumebakia nafasi10 za upendeleo za Rais ambapo litafanya baraza hilo kuwa na wajumbe 88 pamoja na spika.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
Karibu sana
LINK
CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: