CHAMA cha Wananchi (CUF) kinahofia mauaji visiwani Zanzibar endapo kitatoa kauli ya kuwataka wanachama na wananchi kusaka haki yao kutoka mikononi mwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Nassor Ahmed Mazrui, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar akizungumza na mtandao huu leo amesema, CUF ina hofu ya Mungu na kwamba, wanajua endapo watakapowafungua minyororo wananchi wao, Zanzibar haitakalika.
Amesema, chama hakioni hoja ya kusababisha mauaji kutokana na dhuluma inayofanywa na Dk. Ali Mohammed Shein, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar na viongozi wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Dunia ukiiendea mbio mwisho wake ni kuangamia, tunajua dhulma huwa haidumu. Inahitajika sana subra ili kuokoa maisha ya wengi. Tunajua kwamba dhulma imetendeka lakini hakuna shaka hakutakuwa na mwananchi atakayeuawa kwa sababu yetu,” amesema na kuongeza;
‘’Sisi tumetulia, hatuna shaka tunatizama tu watakachoamua kufanya sisi tutakaa kimya kwani hatuko tayari wananchi wetu wamwage damu.”
Mazrui amesema kuwa, kwa sasa wananchi wengi wanaweza kutojua kwanini CUF imekaa kimya na kwamba “kukaa kimya pia si ujinga, muda ukifika wananchi wataelewa kwa nini tuliamua kujitoa kwenye uchaguzi na kukaa kimya.’’
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA


No comments: