Madai ya unyanyasaji wa kingono nchini Iran katika kituo kimoja cha runinga yamesababisha wanawake nchini Iran kuvunja ukimya wao na kuanza kulijadili swala hilo kwa kina ambalo kwa utamaduni wao ni mwiko.
Sheena Shirani,msomaji habari katika runinga ya Press TV ambayo hutumia lugha ya kiingereza ,alivunja mwiko huo kwa kuzungumza unyanyasaji wa kingono aliokumbana nao mbele ya wasimamizi 2 wa kituo hicho kwa kipindi kirefu
Madai yake yalisambazwa hadharani wakati alipochapisha mtandaoni mazungumzo ya simu ambayo mtu anayedaiwa kuwa msimamizi wake kazini Hamid Reza Emadi mara kadhaa alitaka kulala naye.
Kufuatia kisa hicho Shirani aliwacha kazi na kuondoka katika taifa hilo na baadaye kuchapisha rekodi hiyo ya sauti ambayo imesikizwa zaidi ya mara 120,000 katika ukurasa wake wa mtandao wa facebook na mtandao mmoja wa habari uliopo nje ya taifa hilo.
Vilevile alichapisha majibizano yake ya maandishi na Emadi ambapo anamtaka kuondoa sauti hiyo katika mtandao wake.
Asante sana kwa kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website hii
Pia waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
Whatsapp / Call - 0652 989 873
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: