Rais Yoweri Museveni amezindua basi la kwanza katika eneo la Afrika mashariki linalotumia nguvu za jua.
Mabasi hayo yalitengezwa nchini Uganda na kampuni ya magari ya Kiira Motors Kayoola.
Yalionyesha mara ya kwanza hadharani katika uwanja wa taifa Kampala mapema mwezi huu.
Moja ya betri zake inaweza kutiwa chaji na vibamba vyenye chaji ya miale ya jua vilivyopo katika paa la magari hayo ambavyo huongeza kasi ya gari hilo kufikia kilomita 80.
Basi hilo lenye viti 35 linatarajiwa kutumika mijini badala ya miji mikuu kutokana na masharti ya umbali wa usafiri wake.
Iwapo yatatengezwa kwa wingi, kila basi linaweza kugharimu dola 58,000 ambayo bwana Musaizi anasema ni bei nzuri katika soko.
Kampuni ya magari ya Kiira Motors ilikuwa kufuatia mradi wake katika chuo kikuu cha Makerere,ambacho kinamiliki hisa katika kampuni hiyo na ambacho pia kimefaidika na fedha za serikali.
Asante sana kwa kutembelea
Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea
kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website
hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website
hii
Pia waweza kuwasilina nasi
au kutufollow hapa chini
Karibu sana
LINK
CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: