Serikali ya Baraza la Jiji la Nairobi imetwaa majengo ya shirika la utangazaji la Kenya (KBC) kutokana na kutolipiwa kodi.
Baraza hilo limeweka bango kubwa katika lango la majengo hayo kutangaza kwamba kwa sasa majengo hayo yamo chini ya usimamizi wa baraza hilo.
"Wapangaji wote wanafaa kulipa kodi kwa Baraza la Jiji hadi malimbikizi ya kodi yalipwe,” tangazo la baraza hilo linasema.
Baraza la jiji linasema linadai kodi ya jumla ya $20 milioni (Shilingi bilioni mbili za Kenya).
Hii si mara ya kwanza kwa baraza hilo kutwaa usimamizi wa majengo jijini Nairobi kutokana na kutolipiwa kodi lakini huwa nadra sana kwa mashirika ya serikali kuandamwa.
Shirika hilo la utangazaji limekuwa likikabiliwa na matatizo ya kifedha miaka ya karibuni.
Asante sana kwa kutembelea
Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea
kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website
hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website
hii
Pia waweza kuwasilina nasi
au kutufollow hapa chini
Karibu sana
LINK
CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: