sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » BREAKIN NEWZZ!!:- SERIKALI YA MAGUFULI KUZIFILISI KAMPUNI 24 ZINAZODAIWA KODI 18.95 BILLION HABARI KAMILI LIVE!!

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeikabidhi Kampuni ya Udalali ya Yono kuwafilisi wateja 24 wanaodaiwa kodi ya Sh bilioni 18.95 baada ya kutorosha makontena ya mizigo yao kwenye 


Bandari Kavu (ICD) ya Azam mwishoni mwa mwaka jana.
Majina ya wadaiwa hayo yametolewa jana kwenye vyombo mbalimbali vya habari, na Kampuni hiyo ya Udalali ya Yono baada ya TRA kuwakabidhi kazi ya kuwafilisi kutokana na kushindwa kutekeleza wajibu wao baada ya kupewa muda wa kulipa kodi.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Yono Kevela alisema wamepewa amri na TRA ya kisheria ya kukamata mali za wadaiwa na kuwafilisi ili kulipia kodi wanazodaiwa.
 

Kevela alisema baada ya kupata kazi hiyo, wao wameona busara kuwatangaza kwenye vyombo vya habari na kuwapa siku 14 kulipa kodi wanazodaiwa na kwamba baada ya muda huo kumalizika, hatua za kukamata mali za wadaiwa hao zitaanza na kuwafilisi.
“Tumekabidhiwa wadaiwa 24 na TRA, hawa wamekwepa kodi kwa kutorosha kontena katika Bandari Kavu ya Azam mwishoni mwa mwaka jana, sasa walipewa muda wa kulipa ila wamekaidi, sasa kazi tumepewa sisi na tutawafilisi mali zao zote ili kulipa deni hilo,” alifafanua Kevela.
 

Majina ya wadaiwa hai na kiasi cha fedha wanachodaiwa kwenye mabano ni Zulea Abas Ali (16,760577.24), Omary Hussein Badawy (21,346,615.40), Libas Fashion (26,593,245.78), Said Ahmed Said (28,249,352.50), Strauss International (45,393,769.95) na Farid Abdallah Salum (52,185, 614.97).
 

Wengine ni Ally Awes Hamdani (55,485,904.07), Nasir Saleh Mazrui (60,105,873.77), Simbo Yona Kimaro (64,221,009.10), Zuleha Abbas Alli (75,508,551.88), Issa Ali Salim (94,543,161.96), Ally Masoud Dama (102,586,719.22), Juma Kassem Abdul (130,182,395.12), Salum Link Tyres (233,447,913.31), Tybat Trading Co. Ltd (448,690,271.90), IPS Roofing Co. Ltd (966,723,692.10) na Tifo Global Trading Co Ltd (1,573,300,644.58).
 

Pia wamo Lotai Steel Tanzania Ltd (5,476,475,738.19), Tuff Tyres General Co Ltd (7,435,254,537.03), Swalehe Mohamed Swalehe (34,687,165.00), Rushwheel Tyre General Co Ltd, (1,802,988,679.20), Said Ahmad Hamdan (68,362,558.31), Ahmed Saleh Tawred (59,237,578.40) na Farida Abdullah Salem (75,334,871. 85).
 

Kevela alisema wadaiwa hao wanapaswa kulipa madeni yao ndani ya siku 14 walizopewa na kwamba iwapo watashindwa kutekeleza amri hiyo, kampuni hiyo itaanza kazi ya kukamata mali zao na kuwafilisi. Alisema ili kurahisisha kazi hiyo, Kampuni ya Said Salum Bakhresa (SSB) ambayo ndiyo mmiliki wa Bandari Kavu ya Azam pamoja na Kampuni ya Regional Cargo Services wanapaswa kutoa ushirikiano kuhakikisha wadaiwa hao wanalipa kodi walizokwepa.
 

“Kampuni hizo zinahusishwa na kutoroshwa kwa kontena 329 zilizokuwa Azam ICD, sasa ni vyema watoe ushirikiano ili wadaiwa walipe fedha za serikali,” alifafanua Kevela. Alisema baada ya muda waliotoa kumalizika, wahusika watapaswa kulipa na gharama za ziada ambazo ni pamoja na faini na usumbufu wa kuwatafuta.
 

Desemba 12, mwaka jana, aliyekuwa Kaimu Kamishna wa TRA, Dk Philip Mpango aliwaambia waandishi wa habari kuwa kampuni 15 kati ya 43 zilizokwepa kodi baada ya kutorosha kontena 329 katika ICD ya Azam, zimelipa.
 

Dk Mpango alisema Desemba 12, mwaka jana ndiyo ilikuwa siku ya mwisho aliyotoa Rais John Magufuli ya siku saba kwa wakwepa kodi hao 43 kulipa wenyewe kwa hiari, vinginevyo sheria zitachukua mkondo wake. Kutokana na kauli hiyo ya Rais Magufuli, wadaiwa 15 walijitokeza na kulipa na waliobaki hawakujitokeza kulipa.




Asante sana kwa kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website hii
Pia waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini

INSTAGRAM           FACEBOOK    GOOGLE +    PINTEREST   TWITTER       

LINKEDIN     DRIBBBLE    NOTJUSTOK



Karibu sana
LINK CLASSIC


BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply