Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Al-Shabab kutoka Somalia limesema ndilo lililoshambulia ndege iliyotoboka shimo ikiwa angani mapema mwezi huu.
Kupitia taarifa iliyotumwa kwa barua pepe al-Shabab wamesema shambulio hilo lilikuwa la kulipiza kisasi operesheni za kijasusi zinazoendeshwa na mataifa ya Magharibi nchini Somalia.
Shimo hilo kwenye ndege hiyo lilitoboka muda mfupi baada ya ndege hiyo kupaa kutoka Mogadishu, ikiwa futi 10,000 (3,048m) juu angani.
Ndege hiyo ilifanikiwa kutua kwa dharura.
Ndege hiyo ya shirika la ndege la Daallo, iliyokuwa ikielekea Djibouti, ilikuwa imebeba watu karibu 60.
Maafisa nchini Somalia baadaye walitoa video inayoonesha watu wawiliwakimkabidhi abiria mmoja anayeshukiwa kuwa mlipuaji wa kujitolea mhanga kitu kinachoonekana kama Laptop kabla ya mlipuaji kuabiri ndege hiyo.
Msemaji wa serikali anasema kuwa watu hao ndio washukiwa wakuu katika ulipuaji huo.
Inasadikika kuwa mmoja kati ya watu walioleta kipakatilishi hicho alikuwa ni mfanyikazi wa shirika linalohudumu katika uwanja huo wa ndege wa Mogadishu.
Watu 20 wamekamatwa wakiwemo wale wawili walionaswa kwenye video hiyo.
Asante sana
kwa kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana
pia endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi
ndani ya Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako
kutembelea website hii
pia waweza
tupia namba yako ukawa unapata habari kupitia simu yako bureeeeeeee...ila simu
iwe smartphone
Pia waweza
kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
Whatsapp / Call - 0652 989 873
Karibu sana
LINK
CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: