Ni Everton, hawa ndio vinara wa kupewa penati katika ligi kuu Uingereza EPL na juzi katika mchezo wao wa EPL vs Swansea ilishuhudiwa wakipewa tuta lao la 7 msimu huu lililowapeleka kilele cha penati.
Penati walizopata Everton zimewaweka juu ya vinara wa ligi kuu Uingereza Manchester Citu ambao hadi sasa wameshapewa zawadi ya mikwaju ya penati mara 5 ikiwa ni mbili nyuma ya Everton.
Leicester, Watford, Brighton and Hove, Crystal Palace na Southampton wanafuatia wakiwa wote wamepiga penati tatu tatu hadi kufikia sasa katika EPL.
Manchester United, Liverpool, West Ham na Arsena wanafuatia wakiwa wana penati mbili mbili huku Chelsea, Stoke City,Fc Bournamouth na Huddersfield town wenyewe hadi sasa wana penati moja moja.
Vilabi vya Tottenham Hotspur, Burnley, West Bromich Albion, Newcastle na Swansea hadi sasa hawajapata bahati ya kupewa zawadi ya pigo la penati hata mara moja.
KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: