“Mimi ni mwanasoka niliyekamilika, mimi ni mwanasoka bora katika historia ya soka nimefanya mengi ambayo sio rahisi kufanyika” huyo ni Cristiano Ronaldo baada ya kutwaa tuzo ya Ballon D Or.
Lakini kiungo wa zamani wa klabu ya Barcelona Xavi Hernandez ameibuka na kusema anashukuru amemuona CR7 akicheza soka na amemuona Lioneil Messi pia lakini akakiri Messi ni hatari kuliko Cristiano.
Xavi anasema katika soka hakujawahi kutokea mchezaji kama Lioneil Messi na Cristiano Ronaldo kama anaona yeye ni bora baasi aamini hivyo lakini watu wanaotazama soka lao wanaona Messi ni zaidi.
Pamoja na uwezo wake wa kutengeneza nafasi awapo uwanjani lakini Xavi anasema Messi ni zaidi kwani huwa uwanjani anafanya vitu ambavyo unaweza kujiuliza kile kakifanyaje na huwa muda wote analenga kuibeba timu.
Jumamosi hii wawili hao wataoneshana umwamba huku Messi akiwa amefunga mabao 18 katika michezo 24 msimu huu na Cristiano Ronaldo akiwa amefunga mabao 16 katika michezo 21 msimu huu.
Barcelona wanaongoza ligi wakiwa na alama 42 kileleni huku wapinzani wao Real Madrid wako nafasi ya nne wakiwa na alama 31 ikiwa ni alama 11 nyuma ya Real Madrid na El Classico inaweza kushuhudia pengo la alama kuongezeka ama kupungua.
KARIBUNI SANA KWA HUDUMA NZURI NA BEI NAFUU
KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: