MWENYEKITI wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Wananchi (CUF) upande wa Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif, Julius Mtatiro na wenzake huenda wakavuliwa uanachama baada ya kudaiwa kukaidi wito wa kamati ya utendaji ya chama hicho.
Wanachama hao waliitwa na Kamati ya Utendaji ya CUF Wilaya ya Ubungo kujibu tuhuma kwanini wasifukuzwe kutokana na mienendo yao ndani ya chama hicho. Mbali ya Mtatiro wengine ni Khalid Singano, Kassim Choga, Mawano Yusuf Kilemi, Jumanne Ally, Mwinyi Khamis na Twaha Rashid.
Katibu wa CUF Wilaya ya Ubungo, Ali Makwilo, amesema kikao hicho kilifanyika jana lakini waliotikia wito huo ni wanachama wawili tu. Aliwataja wanachama walioitikia wito huo kuwa ni Katibu wa Tawi la Kimara Stop Over, Yahaya Muhsin na Katibu wa Tawi la Matangini, Patrick Mwakasege.
“Ni kweli tumewaita na wapo waliokuja lakini Mtatiro na wenzake hawakuja, maana yake wamedharau wito. Kisheria ukituhumiwa halafu hukwenda unaruhusu mamlaka ikuadhibu,” alisema Ali Makwilo.
KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: