Licha ya Alikiba kushindwa kutokea kama ‘Special Appearance’ katika show ya ufunguzi wa JS Hotel mjini hapo lakini mdogo wake ambaye ndiye alikuwa na show Abdukiba alikinukisha na kuwakosha mashabiki waliotokeza kwenye ‘party’ hiyo. 
Abdukiba akikinukisha.
“Juzi nilitakiwa kujiunga na mashabiki wangu wa chato Geita,  nyumbani kwa Baba yetu Muheshimiwa Rais lakini nilishikwa na homa kali ila leo naendelea Vizuri samahani kwa kutokuwepo lakini nawaahidi nitarudi tena kwa nguvu zote Mungu akipenda hivi karibuni tutawaandalia show ya kipekee lakini vilevile Abdukibaa mdogo Wangu aliniwakilisha vema namshukuru sana ” aliandika Alikiba.
Muonekano wa JS Hotel.
Mbali na hilo Alikiba amedai hali yake kiafya sasa iko poa kwani anaendelea vyema na kudai wanajipanga kuona jinsi gani wanaweza kufungua mwaka vizuri 2018 kutokana na kuugua kwake kuharibu mipango yake ikiwa pamoja na kushindwa kufanyika kwa funga mwaka na Alikiba.

KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA


 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 








 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments: