sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » ALIYEKATWA MASIKIO KWA KUMLAWITI MTOTO ATIWA NGUVUNI


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga  Simon Haule amethibitisha kuwa Jeshi la Polisi Mkoani kwake linamshikilia kijana Msigala Salum (24) kwa tuhuma za kumlawiti mtoto  mwenye umri wa miaka mitatu.


Kamanda Haule  amesema Kijana  huyo aliyejulikana kwa jina la Msigala Salum (24) amekatwa masikio yote mawili na wananchi wenye hasira kali baada ya kumlawiti mtoto huyo mwenye umri wa miaka mitatu katika eneo la Majengo Mapya Kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga.

"Tukio hilo limetokea Disemba 20, 2017 majira ya saa tatu asubuhi ambapo kijana huyo anayejishughulisha na shughuli ya kuosha magari mkazi wa Ndala, alimdanganya mtoto huyo wakati akicheza na wenzake nyumbani kwao, kutokana na tukio hilo mtuhumiwa alishambuliwa na wananchi kabla ya Jeshi la polisi kufika eneo la tukio na kumuokoa", amesema Kamanda Haule.

Aidha kamanda Haule ameongeza kwa kusema kuwa mara baada ya tukio hilo baba mzazi wa mtoto huyo alimkamata mtuhumiwa na kumkata masikio yote mawili kwa kutumia kisu na kukimbia, na jeshi la Polisi bado linaendelea kumtafuta.


KWA HABARI ZAIDI

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply