Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta kesho anatarajia kufanyiwa upasuaji wa goti baada ya kuumia hivi karibuni akiitumikia klabu yake ya KRC Genk ambayo inashiriki ligi kuu ya soka ya Ubeligji.
Taarifa ya Shirikisho la soka nchini TFF, imesema Samatta kesho atafanyiwa upasuaji mkubwa wa goti na jopo la madaktari wa klabu ya Genk.
“Mbwana Samatta atafanyiwa upasuaji wa goti kesho na jopo la madaktari na baada ya upasuaji matibabu yatachukua wiki nane hivyo atakuwa nje ya uwanja kwa muda wote huo”, amesema Alfred Lucas msemaji wa TFF.
Aidha Alfred amesema madaktari wamekadilia kuwa Samatta anaweza kurejea uwanjani Januari 10 mwakani ambapo timu ya taifa itamkosa katika michezo kadhaa ikiwemo michuano ya Challenge inayotarajiwa kufanyika Januari mwakani.
Kwa upande wa mchezo wa Novemba 12 ambapo Taifa Stars ipo ugenini kuivaa Benin utaanza majira ya saa 12:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki huku kikosi hicho kikiwa kimeongezewa nguvu na wachezaji Farid Mussa pamoja na Mbwana Samatta.
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: