sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » RAIS MUGABE APEWA MASAA KUJIUZULU URAIS ZIMBABWE


Baada ya kuvuliwa nafasi ya kiongozi wa juu wa Chama cha Zanu- PF Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amepewa masaa tu na Chama hicho kujiuzulu mwenyewe kwenye nafasi ya Urais wa nchi hiyo bila kutumia nguvu.

Chama tawala nchini humo leo baada ya kutangaza kuwa kimemvua uongozi Rais huyo mkongwe zaidi barani Afrika, Robert Mugabe, kimemwambia hadi kesho saa 6 mchana awe tayari ametangaza kujiuzulu nafasi ya Urais huku kikimuonya kuwa endapo atakaidi nguvu ya ziada itatumika kumng’oa madarakani.

“Rais wetu wa zamani, Robert Mugabe amepewa muda hadi kesho jumatatu saa 6 mchana awe ameshatangaza kujiuzulu nafasi ya Urais wa Zimbabwe la sivyo nguvu itatumika kumng’oa madarakani.”Imeeleza taarifa kutoka kwenye chama cha Zanu-PF iliyochapishwa kwenye ukurasa wao rasmi wa Twitter.

Nafasi ya Rais Mugabe itachukuliwa na kiongozi mkuu wa Chama tawala cha Zanu PF aliyechaguliwa leo kwenye kamati kuu ya chama hicho, Emmerson Dambudzo Mnangagwa ambaye pia alishawahi kuwa Makamu wa Rais wa Mugabe kabla ya kutimuliwa.

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply