Watu kadhaa wanasadikika kufariki na wengine kujeruhiwa kwenye ajali ya gari iliyotokea mchana huu mkoani Kilimanjaro ikihusisha roli na gari ndogo aina ya Noah ya abiria ya Sanya Juu - Moshi
Ajali hiyo mbaya imetokea mchana huu maeneo ya Kikavu karibu na Kwasadala Mkoani Kilimanjaro ambapo Roli kubwa lilikuwa linajaribu kulipita gari lingine ndipo likakutana uso kwa uso na Gari ndogo aina ya Noah iliyokuwa imebeba abiria likitokea Moshi mjini kwenda Sanya Juu.
Taarifa kamili za ajali hiyo bado hazijatolewa lakini mashuhuda wa tukio wanasema huenda baadhi ya abiria waliokuwa kwenye Noah wamejeruhiwa.
Aidha mashuhuda hao wameeleza kuwa watu wanne ndio wanaonekana kuwa bado ni majeruhi lakini hali zao ni mbaya na taratibu za kuwafikisha hospitali kwaajili ya matibabu zinaendelea.
Hata hivyo bado majina ya abiria waliokuwemo kwenye Noah hayajapatikana mara moja tunaendelea kufuatilia taarifa kamili kutoka kwa kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro na tutaendelea kuwajulisha.
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: