UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI
Jana usiku KRC Genk ikiwa ugenini ilishuka dimbani ikikaribishwa na Gent zote za nchini Ubelgiji katika mchezo wa Europa League hatua ya 16 bora.
Mchezo huu ulipigwa katika dimba la Ghelamco lenye uwezo wa wa kuingiza watu 17,000 ambapo ndani ya dakika 90 Genk iliisambaratisha Gent kwa jumla ya magoli 5-2 na kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua inayofuata.
Katika mchezo huo, mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Tanzania anayekipiga katika klabu ya Genk, Mbwana Samatta alifanikiwa kupachika kimiani magoli mawili.
Goli la kwanza la Samatta alilifunga dakika ya 41 baada ya kupokea pasi kutoka kwa J. Boetius huku goli la pili likifungwa dakika ya 72 baada ya kupokea mpira toka kwa Thomas Buffel.
Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana
Karibuni sana
LINK CLASSIC
LIKE PAGE ZETU
"KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: