UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI
Kupoteza kumbukumbu ni ugonjwa unaoingia kwa kasi ugonjwa Umetajwa sasa unakuja juu kuliko maradhi sugu kama vile kisukari, shinikizo la damu, kiharusi na saratani
Kupoteza kumbukumbu hutokea pale eneo la ubongo linalohusika katika kuhifadhi taarifa linapoathirika.
Ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu kwa kawaida unawapata wazee. Uligunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1906 na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akili, Alois Alzheimer.
Dk Alzheimer, ambaye ni MjerumU ani, alipata mgonjwa mwenye tatizo hilo ambaye alikuwa anapoteza kumbukumbu, kuchanganyikiwa na kupata ugumu wa kuelewa maswali anayoulizwa.
Mgonjwa huyo alifariki dunia na ndipo Dk Alzheimer alipofanya uchunguzi katika ubongo wa marehemu na kubaini kuwa kulikuwa na hitilafu katika baadhi ya seli za ubongo wake.
Hivyo, akawa daktari wa kwanza kubaini ugonjwa huo wa kupoteza kumbukumbu na kulifanya Shirika la Afya Duniani (WHO) limpe heshima kwa kuuita ugonjwa huo jina la daktari huyo. Ugonjwa huo unafahamika kama Alzheimer.
Ugonjwa huu ni moja ya matatizo makubwa ya kiafya yanaoikabili dunia hasa katika kipindi hiki ambacho kuna ongezeko la wazee hasa katika nchi zilizoendelea.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, mnamo mwaka 2010 ugonjwa huu ulishika namba ya sita kati ya magonjwa yanayosababisha vifo nchini Marekani.
Ripoti WHO kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Kupambana na Ugonjwa wa Alzheimer (ADI), inakadiria kuwa idadi ya wagonjwa wa tatizo hili itaongezeka mara tatu zaidi ifikapo mwaka 2050 na kuifanya dunia kuwa na wagonjwa zaidi ya milioni 135.
WEWE NI MIONGONI MWA WATU HAO? Siyo jambo la ajabu lakini unapaswa kutunza afya yako.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo kwa sasa kuna watu 44 milioni wanaougua maradhi haya hatari duniani kote. Idadi hii ni sawa na ongezeko la asilimia 22 ya wagonjwa 35.6 milioni waliokuwa na maradhi haya miaka mitatu iliyopita.
Wataalam wanasema, “Ugonjwa huu ni janga la kimataifa na hali inazidi kuwa mbaya. Tunapoangalia hali ya siku za usoni, tunaona kuwa idadi ya wagonjwa itaongezeka sana.” ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu miongoni mwa wazee, ni moja ya magonjwa yanayowakabili watu wenye umri zaidi ya miaka 55 na unasababisha upotevu wa mapato kuliko saratani, kiharusi na magonjwa ya moyo kwa pamoja.
Ugonjwa huu wa wazee, unasababisha mtu kupoteza kumbukumbu ya matukio ya karibuni na kadri ugonjwa unavyoendelea mtu anaweza kushindwa kuzungumza vizuri. Tatizo jingine ni kupoteza uwezo wa kuelewa mazingira anayoishi, kushindwa kujihudumia na kupata mabadiliko ya kitabia kama vile kujitenga na watu wa familia au jamii.
Ingawa hali hii hujitokeza taratibu, lakini inaweza kusababisha kifo ndani ya kipindi cha miaka mitatu hadi tisa. Hii ni kwa mujibu wa utafiti wa S. Todd na wenzake uliochapishwa mwaka 2013 katika jarida la International Geriatric Psychiatry, toleo la 28 (11).
Ingawa chanzo halisi cha maradhi haya hakijulikani bayana, baadhi ya wanasayansi wanaamini kuwa ugonjwa huu unatokana na changamoto za mazingira pamoja na matatizo ya urithi wa vinasaba vya kijenetiki vyenye mwelekeo wa kupata tatizo hili.
Wataalamu wa afya wanaamini chembe za urithi zinachangia kutokea kwa maradhi haya kwa asilimia 70. Katika utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa katika jarida la kisayansi la Nature Genetics, ilibainika kuwa kuna takriban aina 20 za vinasaba vya kijenetiki vinavyochangia mtu kupata maradhi haya.
Timu ya watafiti wa taasisi ya Pasteur ya nchini Ufaransa iliyoongozwa na Philippe Amouyel ilipata ushahidi kutoka kwa washiriki wa utafiti zaidi ya 74,000 kutoka nchi 15 sehemu mbalimbali duniani na kubaini kuwa wagonjwa wenye maradhi haya, DNA zao zilikuwa na matatizo yanayofanana.
Mambo mengine yanayotajwa na wanasayansi kuwa yanachangia mtu kupata maradhi haya ni pamoja na shinikizo la damu, msongo wa mawazo pamoja na ajali zinazohusisha kichwa.
Maradhi haya yanaweza kugundulika kwa daktari kuchukua maelezo ya tatizo, historia ya kitabibu, kufanya jaribio la kupima uwezo wa mtu wa kiakili, kupima damu na vipimo vyingine vya uchunguzi kwa kutumia mionzi kama vile MRI.
Kwa ujumla, maradhi haya hayana tiba ya moja kwa moja yanayofanya mgonjwa alirudie hali yake ya kiakili kama awali, ingawa kuna dawa zinazosaidia mtu kukabiliana na dalili za maradhi kama vile msongo wa mawazo.
Mazoezi ya mwili ni muhimu katika programu ya tiba ya wagonjwa wa namna hii ili kuzuia hali isiwe mbaya haraka na kumkinga mgonjwa dhidi ya maradhi yanayowanyemelea watu.
Ulaji wa matunda, mbogamboga, kokwa na nafaka zisizokobolewa pamoja na vyakula vingine ambavyo havijasindikwa, inaweza kuwa njia bora ya kukabili vyanzo vya tatizo hili.
Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana
Karibuni sana
LINK CLASSIC
LIKE PAGE ZETU
"KWA HABARI ZAIDI"
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: