UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA
Baadhi ya maofisa wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) waliokuwa kwenye mashine za ukaguzi Rais John Magufuli alipofanya ziara ya ghafla uwanjani hapo wameondolewa kwenye kitengo hicho.
Majina ya maofisa hao yamepelekwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ili wachukuliwe hatua.
Waziri wa wizara hiyo, Profesa Makame Mbarawa ameambiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (Taa), George Sambuli kuwa maofisa hao wameondolewa uwanjani hapo.
Sambuli amesema: “Wale watumishi waliokuwapo pale tulichukua hatua za awali za kuwahamisha,pia tuliandika taarifa na kuipeleka wizarani tunasubiri maelekezo zaidi.”
Awali, maofisa hao walitoa majibu yanayotofautiana kuhusu mashine ya ukaguzi iliyopo kitengo cha ukaguzi wa mizigo.
Amesema wamejitahidi kushughulikia wizi wa mafuta ya ndege uliokuwapo katika maeneo ambayo hayakuwa na kamera baada ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuchukua hatua.
Profesa Mbalawa amesema taarifa hiyo haijamfikia mezani kwake kwa kuwa alikuwa katika vikao vya Bunge mjini Dodoma.
“Tumeamua kufanya ziara na Katibu wa Wizara ili kuona maelekezo aliyotoa Rais, tumeona mashine zote zinafanya kazi, lakini tunaangalia mafanikio na changamoto ambazo wanakabiliana nazo,” amesema
Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana
+255 (0) 652989873 – Whatsapp / Call
Karibuni sana
LINK CLASSIC
LIKE PAGE ZETU
"KWA
HABARI ZAIDI "
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: