UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema ujenzi wa bandari mpya kwa Mpigaduri ndiyo suluhisho la kumaliza msongamano wa bidhaa mbalimbali, ikiwemo makontena katika bandari ya sasa ya Malindi.
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Usafiri, Uchukuzi na Miundombinu, Mohammed Ahmada Salum wakati akijibu hoja za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliotaka ufafanuzi kuhusu masuala ya bandari.
Alisema ni kweli bandari ya Malindi imezidiwa na msongamano wa bidhaa mbalimbali yakiwemo makontena na hivyo kukosekana kwa nafasi ya kutosha ikiwemo meli zinazotoka kushusha bidhaa.
“Tatizo la ufinyu wa nafasi katika bandari ya Malindi linafahamika na suluhisho lake ni kukamilisha mradi wa ujenzi wa bandari mpya kwa mpigaduri huko Maruhubi,” alisema.
Alieleza mchakato wa ujenzi wa bandari hiyo unaendelea ambapo hivi karibuni wataalamu kutoka China walifika nchini ili kuchukua sampuli ya udongo katika eneo la ujenzi wa bandari.
Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana
+255 (0) 652989873 – Whatsapp / Call
Karibuni sana
LINK CLASSIC
LIKE PAGE ZETU
"KWA
HABARI ZAIDI "
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: