sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » KESI YA TUNDU LISSU YASOGEZWA HADI JULAI 14

UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), amepandishwa kizimbani baada ya kujisalimisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, kujibu tuhuma za kuchapisha chapisho la uchochezi lenye kichwa cha habari’ Machafuko yaja Zanzibar’.

Lissu alifika mahakamani hapo kwa ajili ya kuitikia wito wa kumtaka kwenda kujibu tuhuma za uchochezi zinazomkabili baada ya washitakiwa wenzake wawili akiwemo Mhariri wa Mawio ambalo lilifungiwa kwa muda usiojulikana, Simon Mkina kusomewa mashitaka.

Mbunge huyo na washitakiwa wenzake Mkina na mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob, walipanda kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Upande wa jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Paul Kadushi kwa kushirikiana na Salim Msemo, ulidai mahakamani hapo kuna washitakiwa Lissu, Mkina na Mehboob na mshitakiwa Jabir Idrisa bado hawajampata na wamepata taarifa anaumwa.

Kadushi aliomba kumsomea mashitaka Lissu, ambapo alimsomea mashitaka matatu ya kula njama kuchapisha chapisho la uchochezi, kuchapisha taarifa yya uchochezi na kosa la tano ambalo ni mbadala wa kosa la pili la kutishia.

Wakili huyo alidai Lissu na wenzake kati ya Januari 12 hadi 14, mwaka huu, Dar es Salaam, walikula njama ya kuchapisha chapisho la uchochezi katika gazeti la Mawio lenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar’.

Lissu alikana mashitaka hayo, ambapo Hakimu Simba alisema Juni 14, mwaka huu, shauri lilipokuja kwa mara ya kwanza upande wa utetezi ulileta pingamizi juu ya uhalali wa mashitaka wakiomba yafutwe. Kesi hiyo itatajwa Julai 14, mwaka huu


Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana
+255 (0) 652989873 – Whatsapp / Call

Karibuni sana
LINK CLASSIC

LIKE PAGE ZETU 



"KWA HABARI ZAIDI "

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply