UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA
Kutoa Zaka ni nguzo ya tatu katika dini ya kiislamu ambapo kiongozi wa dini hiyo Mtume (Swalla Llahu alayhi wa sallam) amesema “Nguzo za Uislam ni tano, Shahada kuwa hapana Mola anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allah, na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Kusimamisha Swala, na Kutoa Zaka, na Kufunga mwezi wa Ramadhan na Kuhiji Makka kwa mwenye uwezo wa kufika huko”.
Kufaridhishwa kwa Zaka ni jambo muhimu na tukufu sana kwa Waislamu kwa sababu ya wingi wa faida yake na kwa ajili ya haja kubwa ya kuwepo kwa jambo hilo, kutokana na masikini na mafakiri wanaohitajia sana msaada wa ndugu zao wenye uwezo, kwani katika Kutoa Zaka uhusiano mzuri unajengeka baina ya Waislam matajiri na Waislam masikini, na hii ni kwa sababu siku zote moyo wa mtu huelekea na kumpenda yule anayemfanyia wema na ihsani Zaka inasaidia pia katika kuzisafisha na kuzitakasa nyoyo
Katika kutoa Zaka au Sadaka kunaizoesha nafsi katika kuwapendelea kheri watu wenye haja na katika kuwaonea huruma na pia kunaipatia nafsi baraka nyingi kutoka kwa Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala, hivyo waislamu wajitahidi kuzingatia hayo kwani watapata malipo makumba kutoka kwa mola wao.
Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana
+255 (0) 652989873 – Whatsapp / Call
Karibuni sana
LINK CLASSIC
LIKE PAGE ZETU
"KWA
HABARI ZAIDI "
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: