sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » JOSEPH MBILINYI HAKUKOSEA KUJIITA ‘SUGU’

UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA

Wabunge wa upinzani Easther Bulaya na Tundu Lissu waliadhibiwa kutokuhudhuria vikao vilivyobaki vya mkutano wa tatu na vikao vyote vya mkutano  wa nne kwa makosa mbalimbali ikiwemo kudharau madaraka ya bunge.

Kwa upande wa  Pauline Geku, Halima Mdee, Zitto Kabwe, Godbless Lema wao wanatumikia adhabu ya kutohudhuria vikao vyote vilivyobaki vya mkutano wa tatu na Mbunge John Heche hatohudhuria vikao kumi vya mkutano wa tatu kwa makosa aliyofanya mkutano wa pili mwezi January.

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi leo anaungana na wabunge wenzake kutumikia adhabu ya kutohudhuria vikao kumi vya bungekwa kile kinachodaiwa ukosefu wa nidhamu baada ya mbunge huyo kuonesha kidole cha kati chenye ishara ya matusi. Ukorofi wake ambao unachagizwa na jina la “SUGU” alilojibatiza vinamfanya kufikia hapa alipo huku akiwanyima haki ya msingi ya uwakilishi Wanambeya Mjini.

Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu, amethibitika kuonesha ishara hiyo kwa wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) waliobaki ndani ya ukumbi wa bunge baada ya kuwasilisha taarifa ya maoni ya kambi ya upinzani Azimio la Bunge la kuridhia mkataba wa kimataifa wa udhibiti wa matumizi ya dawa na mbinu za kuongeza nguvu katika michezo, lililowasilishwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.

Sugu amekuwa miongoni mwa wabunge wanaofahamika kwa kusababisha vurugu bungeni kiasi cha kufukia hatua ya kutolewa nje ya ukumbi wa bunge chini ya ulinzi mkali wa askari wa bunge tangu awe Mbunge wa Mbeya Mjini.


Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana
+255 (0) 652989873 – Whatsapp / Call

Karibuni sana
LINK CLASSIC

LIKE PAGE ZETU 



"KWA HABARI ZAIDI "

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply