UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA
OFISI ya Bunge imesema kuwa hali ya Spika wa Bunge, Job Ndugai (pichani) ni njema kabisa na yupo nchini India kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake kutokana na maelekezo ya daktari wake kumtaka hivyo mapema mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano, Ofisi ya Bunge mjini Dodoma jana, kumekuwa na taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu hali ya Spika Ndugai na kuzua hofu kwa viongozi na wananchi.
“Ofisi ya Bunge inapenda kuchukua fursa hii kuwafahamisha Watanzania wote kuwa taarifa hizo ni za uzushi mkubwa na hazina ukweli wowote,” ilieleza taarifa hiyo. Ilieleza kuwa Spika amepokea salamu nyingi za kumtakia kheri wakati akiendelea na uchunguzi wake, kutoka kwa viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge na amewatakia Mfungo mwema wa Ramadhani kwa wale waliofunga kutimiza ibada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
“Mheshimiwa Spika pia amewatakia kazi njema wabunge wote ya kushughulikia Bajeti ya Serikali inayosomwa leo (jana),” ilieleza taarifa hiyo na kuongeza:
“Tunawaomba Watanzania wote wenye nia njema na Spika wetu waendelee kupuuza taarifa zinazotolewa kupitia mitandao ya kijamii na waendelee kumwombea ili afya yake iimarike haraka na kurejea nchini mapema.”
Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana
+255 (0) 652989873 – Whatsapp / Call
Karibuni sana
LINK CLASSIC
LIKE PAGE ZETU
"KWA
HABARI ZAIDI "
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: