UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema CUF haina hatimiliki ya kuongoza Zanzibar, ambapo watendaji na watumishi wa Serikali huko Pemba wametakiwa kuheshimu Serikali iliyopo madarakani kwani imechaguliwa kihalali.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri asiye na Wizara maalumu, Said Soud Said wakati akichangia bajeti ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalumu za SMZ katika Baraza la Wawakilishi.
Soud ambaye ni Mwakilishi wa kuteuliwa na Mwenyekiti wa chama cha AFP alisema wapo watendaji na watumishi wa Serikali wamekuwa wakifanya vituko kwa madai kwamba Serikali iliopo madarakani hawaitambui.
Alisema watendaji wa aina hiyo watachukuliwa hatua za kisheria kwa sababu wanakwenda kinyume na sheria za nchi. “Wapo watendaji kule Pemba wanahitaji kutumbuliwa majipu kwa sababu wanajidai kwamba hawajapata Serikali wanayoitaka…….
Serikali hii ya rais Dk Ali Mohamed Shein imechaguliwa kihalali kwa mujibu wa katiba,” alisema Soud. Alifahamisha kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais Dk Ali Mohamed Shein inaendelea na majukumu yake na kuwataka wananchi kuiunga mkono katika utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Alisema ipo dhana kutoka kwa baadhi ya wananchi ikiwemo wafuasi wa CUF kwamba Serikali iliyopo madarakani haiwezi kupiga hatua na kwenda bila ya CUF.
“Mimi nawaambia wananchi kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo madarakani chini ya Rais Shein na inatekeleza majukumu yake vizuri……hawa CUF wanatakiwa kutambua kwamba hawana hatimiliki ya Zanzibar kwamba kama hawamo serikalini basi hakuna kitakachofanyika,” alisema Soud.
Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana
+255 (0) 652989873 – Whatsapp / Call
Karibuni sana
LINK CLASSIC
LIKE PAGE ZETU
"KWA
HABARI ZAIDI "
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: