
UNGANA NA
LINK CLASSIC
KATIKA KIPENGELE CHA
HOT NEWZ
MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema jukumu kubwa la nchi za ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika ni kuhakikisha zinaweka mazingira mazuri ya kuwezesha wanawake kiuchumi.
Samia aliyasema hayo mwishoni mwa wiki kwenye ufunguzi wa mkutano kuhusu masuala ya kuwezesha wanawake kiuchumi kwa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo uliandaliwa na Jopo la Ngazi ya Juu la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliloliteua mwanzoni mwa mwaka huu kwa ajili ya kusaidia kufanya uchambuzi na kutoa mapendekezo ya namna ya kuchagiza kasi ya kuwezesha wanawake kiuchumi kupitia utekelezaji wa Ajenda 2030 ya Maendeleo Endelevu.
Jopo hilo lenye viongozi na wataalamu mbalimbali, Samia akiwa miongoni wa wajumbe wa jopo hilo, limezinduliwa Machi 15, mwaka huu sambamba na mkutano wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Wanawake.
Makamu wa Rais alisema pamoja na kuwepo kwa jitihada mbalimbali za kuinua wanawake kiuchumi bado mazingira hayampi nafasi na hasa kwa wanawake wa ngazi za chini, wengi wao wakiishi vijijini kutokana na changamoto zinazokwamisha jitihada hizo.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa kutembelea Website hii coz
ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea kusoma na kufungua
LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website hii bila kusahau
kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
Whatsapp
+255 652 989 873
Karibu
sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: