WAKALA wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) na wadau wake wameagizwa kuzimaliza changamoto zinazochelewesha kuanza kwa mradi huo ili huduma ya usafiri ianze haraka iwezekanavyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene alitoa agizo hilo katika kikao chake na uongozi wa Wakala pamoja na wadau wake.
“Kuna baadhi ya changamoto ndogondogo zimebaki…nimetaka wazimalize haraka ili mabasi yaanze kutoa huduma,” Simbachawene aliwaambia waandishi wa habari mara baada ya kikao hicho. Mradi huo uliosubiriwa kwa muda mrefu unatarajiwa kuanza mwezi huu.
Aliwataja baadhi ya wadau wanaotakiwa kufanya kazi na wakala huo kuhakikisha kuwa mradi unaanza kuwa ni Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Wakala wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA), Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Wakala wa Serikali Mtandao (EGA), Msajili wa Hazina, UDA-RT na MAXCOM.
Changamoto zinazotakiwa kutatuliwa kwa haraka ni pamoja na kukwama kwa baadhi ya vifaa vya mradi kutokana na kutolipiwa katika Mamlaka ya Mapato (TRA), kuweka mifumo ya nauli na kadi zake, umeme, kujenga uzio katika vituo, kuongeza ulinzi na ofisi ya kuongozea mabasi.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: