Ungana
na LINK CLASSIC katika kipengele
cha
HOT NEWZ
topic ni
SERIKALI YATENGA BAJETI YA BILIONI 251 KWA AJILI YA DAWA
SERIKALI ya Rais John Magufuli imeongeza bajeti yake ya kununua dawa kutoka Sh bilioni 41 kwa mwaka 2014/15 hadi Sh bilioni 251 mwaka huu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema lengo la hatua hiyo ni kudhibiti uhaba wa dawa nchini.
Alisema hayo wilayani Kahama mkoani Shinyanga , alipoelezea upatikanaji wa dawa nchini baada ya kuzindua kampeni ya kitaifa ya kupima Virusi Vya Ukimwi (VVU) kwa wasichana.
Uzinduzi huo ulifanyika viwanja vya Shule ya Msingi Kakola wilayani hapa. Ummy alisema Serikali ya Awamu ya Tano, itahakikisha hakuna mgonjwa atakayekufa kwa kukosa dawa, kwani katika bajeti ya mwaka huu imetenga fedha za kutosha kwa ajili ya kununua dawa.
“Bajeti ya dawa imeongezeka kutoka shilingi bilioni 41 hadi kufikia shilingi bilioni 251 hii inadhihirisha kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga vyema kuwahudumia wananchi wake, ama hakika Hapa ni Kazi tu,” alisema.
Aliwahakikishia vijana wa kike waliojitokeza kwa wingi kupima afya zao kuwa hakuna atakayekosa dawa baada ya kugundulika ameathirika na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: