Ungana
na LINK CLASSIC katika kipengele
cha
HOT NEWZ
topic ni
BALOZI IDDI ATOA NASAHA KWA WASOMI WA UONGOZI
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amewataka wahitimu wa mafunzo ya uongozi mdogo kutumia mafunzo waliyoyapata ili kuleta mageuzi makubwa ya utendaji katika sehemu zao za kazi.
Balozi Seif aliyasema hayo katika sherehe za ufungaji wa mafunzo ya Jeshi la Polisi ngazi ya Koplo, Sajini na Staff Sajini yaliyofanyika kwenye Viwanja ya Polisi Ziwani mjini Zanzibar. Alisema kuyatumia mafunzo hayo vizuri katika utendaji wa kazi itawezesha kupunguza uhalifu na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi.
“Nategemea mtabadilika na kuwa watendaji wazuri wanaochukia rushwa, kesi zitaendeshwa kwa haraka, haki itatendeka katika kutekeleza majukumu na haki za binadamu zitazingatiwa kwa lengo la kujenga heshima ya Serikali na kuleta uhusiano wa karibu baina yenu na wananchi,” alisema Balozi Seif.
Aidha, alilitaka Jeshi la Polisi kutopuuza uhalifu mdogo mdogo kwani uhalifu huo hatimaye husababisha uhalifu mkubwa na kusababisha uvunjifu wa amani katika nchi.
Naye Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omar Makame aliwakumbusha wahitimu hao kuwa wana wajibu mkubwa wa kuwalinda raia na mali zao pamoja na kulinda sheria za nchi.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
+255
(0) 652989873 whatsapp
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: