Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza kuhusiana na kuaza operesheni ya kuwaondoa ombaomba waliokandokando ya barabara, jijini Dar es Salaam leo.
Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo, mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutoa agizo la kuwaondo watu wanao ombaomba kandokando ya barabara jijini Dar es Salaam.Picha na Michuzi Blog)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema kuwa katika kuweka jiji hilo safi imejipanga kuanza na mambo matatu ambayo ni kuwaondoa ombaomba wa barabarani, kuwabana wamiliki wa majengo makubwa yaliyojengwa kinyume na taratibu pasipokuwa na sehemu za kuegeshea magari na kuwaamuru wamiliki wa bar kutopiga muziki nje ya utaratibu wa vibali vyao.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa ombaomba walikuja Dar es Salaam kwa nauli zao hivyo lazima warudi walikotoka kwa nauli zao.
Makonda ametoa siku sita mpaka April 18 ombaomba ndani ya jiji la Dar es salaam wawe wameondoka
Kuhusu wamiliki wa Bar, Makonda amesema wamiliki wa bar wanaowapigia watu kelele wafuate sheria walizopewa kama ni mwisho saa sita kupiga muziki iwe hivyo na muziki huo upigwe kwenye maeneo husika.
Amesema mtu ambaye anapiga muziki nje ya utaratibu wa kibali chake maana yake ajiandae kunyang’anywa leseni na kufutiwa kibali chake na faini hiyo atailipa mwenyewe.
Aidha, Makonda amewataka wamiliki wa majengo makubwa yaliyojengwa kinyume na taratibu pasipokuwa na sehemu za kuegeshea magari walipe faini na kuweka utaratibu wa kupaki wapi magari yao au kubomoa majengo yao.
LINK
CLASSIC: Asante sana kwa kutembelea Website hii coz
ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea kusoma na kufungua
LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website hii bila kusahau
kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
Whatsapp
+255 652 989 873
Karibu
sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA




No comments: