sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » MADHARA YA KUTOA MIMBA


Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Vingunguti, Dk Modest Mwinuka anasema wanawake wengi wanaofika hospitalini hapo wanadai kuwa mimba imetoka yenyewe wanaogopa kusema ukweli kwa kuhofia kukosa huduma.


Dk Mwinuka anasema moja wapo ya madhara makubwa ambayo yanampata mwanamke anayetoa mimba vichochoroni ni kutoka kwa damu nyingi na kupasuka kwa kizazi.

“Madhara ya baadaye ni kupata maambukizi katika viungo vya uzazikuharibikiwa mimba kila wakati kutokana na shingo ya kizazi kulegea pamoja na kupata msongo wa mawazo,” anasema Dk Mwinuka.

Anasema kuwa madhara mengi ni kupata shida wakati wa kuzaa kwa sababu shingo ya kizazi inakuwa imepata majerahakupata ugonjwa wa Anemia kutokana na kutoka damu nyingi na pamoja na kupata shida ya kushindwa kupata mimba kutokana na maambukizi katika viungo vya uzazi.

“Vilevile kuna madhara mengine ambayo ni mwanamke kupata ugumbamimba kutunga nje ya kizazikuzaa watoto wasio kuwa na akili nzurikupata kansa ya mlango wa kizazi na kuathirika kisaikolojia,” anaongeza.

Muuguzi wa Chama cha Wauguzi nchini (Prinmat), Joseph Siga anasema mfuko wa uzazi una utando maalumu ambao hufanya mimba iliyotungwa kwenye mirija iitwayo fallopian kuwezesha yai kushuka hadi kwenye mifuko ya uzazi, Lakini utoaji wa mimba huambatana na magonjwa ya mirija hiyo na kupoteza utando huo na kusababisha mimba kukulia nje ya kizazi na matibabu ya tatizo hilo ni kukata mrija husika husababisha kuongeza hatari ya ugumba.

“Wanawake wanaotoa mimba wana hatari kubwa ya kupata kansa ya mlango wa uzazi kuliko wengine ambao hawajatoa mimba na hii ni kwa sababu ya kusumbuliwa kwa mlango huo kwa dawa za kutoa mimba, vifaa vya kutoa mimba na mabadiliko ya ghafla ya homoni za uzazi,” anasema Siga.

Anasema baadhi ya njia zisizo salama zinazotumika kuwa ni pamoja vyuma vyenye ncha kali kama spoku za baiskeli, mikasi, utomvu wa mti wa muhogo na vidonge.

Siga anasema idadi kubwa ya wanaotoa mimba kiholela, hupata madhara mbalimbali ikiwamo kutoboka utumbo, kuchanika kwa kizazi, kuoza na wengine kuharibu figo.

Utafiti uliofanywa mwaka 2011 na Shirika la Afya Dunia (WHO) umeonyesha kuwa msichana mmoja kati ya wanne hutoa mimba kwa njia za kienyeji na kati ya mimba 210 milioni zinazopatikana kila mwaka, 46 milioni sawa na asilimia 22 hutolewa.

Ripoti hiyo inabainisha kuwa mwanamke mmoja hufa kila baada ya dakika nane kutokana na matatizo ya utoaji mimba usio salama.


LINK CLASSIC: Asante sana kwa kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website hii
Pia waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini




TWITTER    

LINKEDIN     DRIBBBLE

Karibu sana


LINK CLASSIC

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply