sponsor

Slider

EMBROIDERY, DTF, & SCREEN PRINTING - T-shirt, Overall, Shirt , Pylon, Kofia Nk..


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » WACHINA WA WIZARA YA AFYA WAPIGWA FAINI YA MIL 17 /- KWA WIZI WA MAJI

   

Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) limewapiga faini ya shilingi milioni 17 raia wa China wanaofanya kazi kwenye wizara ya afya (Chinese medical team) baada yakubaini wizi mkubwa wa Maji kwenye nyumba wanayoishi iliyopo mtaa wa Mtwara Oysterbay Jijini Dar es salaam.

Akizungumza kwenye eneo la tukio Meneja wa Dawasco Kinondoni, Bi Judith Singinika alieleza kuwa waliwabaini baada ya kufanya operesheni maalum kwenye mtaa huo ya kubaini wizi wa Maji ndipo walipofanikiwa kunasa nyumba hiyo ikiwa imeunganishiwa Maji pasipo mita na kukuta imefungwa pampu kubwa ya kuvuta Maji kutoka kwenye laini ya bomba kubwa la Maji.

“Dawasco tumewapiga faini raia wa China kiasi cha shilingi milioni 17 baada yakuwanasa wamejiunganishia huduma ya Maji kinyume na utaratibu na laini inayopeleka Maji ndani haina Mita na imefungwa pampu kubwa yakuvuta Maji wakati sio utaratibu hivyo tumeng’oa pampu na nakuwapiga faini ambapo wanatakiwa wailipe ndani ya miezi 24 hivyo watatakiwa walipe kiasi cha shilingi laki 7 kila mwezi”,alisema Singinika.

Hata hivyo meneja wa Dawasco amesisitiza kuwa operesheni hiyo yakukamata wezi wa Maji kwenye maeneo tofauti ya Jijini Dar es salaam niendelevu na inatokana na agizo la Waziri wa Maji na umwagiliaji Mh Gerson Lwenge ambapo alilitaka shirika hilo kukagua majengo yote makubwa pamoja na viwanda nakujiridhisha matumizi yake ya Maji.

Hivyo Dawasco inaendelea kuwasihi watu wote waliojiunganishia huduma ya Maji kiholela kinyume cha utaratibu kwenye nyumba za makazi, majengo makubwa pamoja na viwanda kujisalimisha nakutambuliwa kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa endapo wakibainika kwani ndio wanaolikosesha Shirika mapato.


Pampu iliyokamatwa na mafundi wa Shirika la Majisafi na Majitaka Jijini Dar es salaam (Dawasco) iliyokuwa ikivuta Maji kutoka kwenye laini ya bomba kubwa la Maji kupeleka kwenye laini ndogo ambayo ilikuwa imeunganishwa kiholela pasipo mita kwenye nyumba wanayoishi raia wa China ambao wanafanyakazi wizara ya Afya (Chinese medical team) eneo la mtaa wa Mtwara Oysterbay Jijini Dar es Saalam

LINK CLASSIC: Asante sana kwa kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website hii
Pia waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini

INSTAGRAM           FACEBOOK    GOOGLE+    

PINTEREST   TWITTER    LINKEDIN     DRIBBBLE

Karibu sana


LINK CLASSIC

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply