Mwenyekiti wa wa Tume ya Uchaguzi Tanzania Jaji Damian Lubuva amewataka wananchi wa Zanzibar kutembea kifua mbele na kwenda kutimiza haki yao ya kikatiba kupiga kura hapo kesho kwa ajili ya kupata viongozi wa kuwaongoza
Jaji Lubuva ameyasema hayo baada ya kuwepo kwa woga miongoni mwa baadhi ya wananchi kwa kuwepo kwa vikosi vya ulinzi na usalama katika maeneo mengi jambo ambalo baadhi ya wananchi wamekuwa wakihoji juu ya kuwepo kwa nguvu kubwa kiasi hicho.
”Usalama upo wa kutosha na suala la kuwepo kwa wanajeshi Zanzibar sii suala geni katika mambo ya uchaguzi wa mataifa mbalimbali lengo ni kulinda amani na usalama wa wananchi hivyo wananchi wasitilie shaka wajitokeze bila uoga”-Amesema Jaji Lubuva.
Uchaguzi wa marudio Zanzibar unarudiwa kesho tarehe 20.03.2016 baada ya uchaguzi wa awali wa tarehe 25.10.2015 kufutwa na tume ya uchaguzi Zanzibar kupitia kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Jecha Salum Jecha kwa vigezo kadhaa kikiwepo cha upinzani kujitangazia ushindi mapema kinyume na sheria.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA


No comments: