WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema Serikali haitaingia tena mikataba yenye kutaka gharama za uwepo wa mtambo wa kuzalisha umeme huku wakiendelea na majadiliano kuibadili mikataba ya zamani yenye gharama hizo.
Alisema gharama hiyo ndiyo chanzo kikubwa cha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuwa na madeni makubwa na sasa wanachofanya ni kuingia mikataba ya kibiashara.
Rais John Magufuli anatarajiwa kuweka jiwe la msingi katika eneo la ujenzi wa Mitambo ya Kinyerezi II, wiki ijayo. Akizungumza katika eneo hilo itakayokuwa na mitambo itakayozalisha megawati 240, alisema ujenzi wake utaanza mwezi huu na serikali imeishatoa fedha zote baada ya Rais Magufuli kusimamia malipo hayo yaliyokwama kwa muda mrefu.
Alisema mtambo huo ni tofauti na wa Kinyerezi I ambao unazalisha umeme kwa gesi pekee na joto linatoa mvuke ambao unapotea tu. Alisema ujenzi wa mtambo huo unaofanywa na makampuni ya Japan kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 344 (Sh bilioni 722) zilizotolewa na nchi hiyo kwa riba nafuu utachukua miezi 28 hivyo mwaka 2018 mwanzoni mtambo huo utaanza kuzalisha umeme.
Akiwa katika mitambo ya kuzalisha umeme ya Kinyerezi I, Muhongo alihoji sababu za megawati 150 kuchelewa kuanza kuzalisha na mpaka sasa kuzalisha megawati 70 pekee. Lakini Mkurugenzi wa Tanesco, Felchesmi Mramba alisema mradi huo utaanza kuzalisha megawati 150 Machi 30 mwaka huu na kueleza sababu za kuchelewa ni pamoja na uhakiki wa mitambo.
Akizungumzia hilo, Muhongo aliwataka Tanesco kuwa waangalifu kwa mitambo yake kwani, inashangaza kuona ikitengenezwa na Wamarekani, wahandisi wanatoka Norway huku bomba la gesi likijengwa na Wachina.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu
mungu akubariki sana pia endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna
vingi vizuri zaidi ndani ya Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa
na marafiki zako kutembelea website hii
pia waweza tupia namba yako
ukawa unapata habari kupitia simu yako bureeeeeeee...ila simu iwe smartphone
Pia waweza kuwasilina nasi
au kutufollow hapa chini
Whatsapp / Call - 0652 989 873
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: