sponsor

Slider

EMBROIDERY, DTF, & SCREEN PRINTING - T-shirt, Overall, Shirt , Pylon, Kofia Nk..


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » NJIA YA KUJUA SIMU FEKI PIA ZIJUE SIMU ZITAKAZO FUNGIWA JUNE MWAKA HUU


Utatambua vipi kama simu yako ni feki?

Utaweza kutambua kama simu yako ni feki kwa kuangalia IMEI namba ambacho ni kifupi cha International Mobile Equipment Identity. Kila simu ina IMEI namba kama utambulisho wa simu husika, hivyo simu isiyokuwa na IMEI namba ni sawa na mtu asiye na jina au gari lisilo na namba ya usajili.

Ili kuweza kujua IMEI namba ya simu yako kuna njia kuu mbili

  • Ya kwanza ni kwa kubonyeza *#06# katika simu yako, hapo simu yako itakuonyesha tarakimu kadhaa katika kioo chako, usihofu hizo ndio IMEI namba za simu yako.
  • Ya pili ni kufungua mfuniko wa nyuma wa simu yako alafu toa betri, chini ya eneo linapokaa betri utaweza kuona IMEI namba za simu yako.
  • Kama simu yako ni ya laini mbili katika njia utakayotumia kama ilivyoelekezwa hapo juu utaona IMEI namba mbili tofauti.
  • Mara nyingi IMEI namba huwa na tarakimu 15
imei   imei01

Jinsi ya kuangalia kama simu yako ni feki

Njia ya Kwanza
  • Baada ya kuangalia IMEI namba yako inakili pembeni, alafu fungua sehemu ya kuandika ujumbe mfupi wa maneno katika simu yako na andika namba uliyoinakili
  • Itume kwenda namba 15090 na subiri muda mfupi utajibiwa ujumbe wako
  • Katika ujumbe utakaojibiwa utakuwa na taarifa za simu kama jina la simu na modeli yake, angalia taarifa hizo kwa makini kama zinafanana na za simu yako, kama zinafanana basi tambua simu yako ni origino na haitafungiwa June 16, ila kama zinatofautiana basi tambua simu yako ni feki na itahusika katika kifungo cha June 16.
Njia ya Pili
  • Kwa kutumia kompyuta au simu yako tembelea tovuti ya Mamlaka ya Mawasiliano kwa kugonga hapa, utapelekwa katika ukurasa wenye fomu ya kujaza IMEI namba za simu yako.
  • Ingiza IMEI namba za simu yako alafu alafu bonyeza kitufe kilichoandikwa Verify My Device
  • Utaletewa maelezo yanayohusiana na simu yako, angalia kwa makini kama maelezo hayo yanafanana na ya simu yako, kama yanafanana basi simu yako ipo safi na haitahusika na kifungo cha Juni 16.
tcra02

Kwanini TCRA wanataka kufungia simu feki zisizo na IMEI namba

Kama nilivyoeleza hapo awali IMEI namba ni utambulisho wa simu katika mtandao hivyo ni muhimu kila simu iwe na IMEI namba halisi. Hebu tuangalie faida za mfumo huu kama ilivyoelezwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini, TCRA.
Mfumo huu wa rajisi una faida zifuatazo:
1. Kuthibiti wizi wa simu. Iwapo mtu atapoteza au ameibiwa simu ya kiganjani na akatoa taarifa kwa mtoa huduma, simu hiyo itafungiwa isiweze kutumika kwenye mtandao mwingine wowote wa simu za kiganjani. Mteja anaponunua simu ni lazima adai risiti halali na halisi na pia garantiii ya angalau miezi 12. Mteja anatakiwa aihifadhi risiti hiyo angalau kwa miezi mitatu. Baada ya hapo, iwapo simu imekuwa inatumika, taarifa za matumizi zinaweza kutumika kama uthibitisho mbadala wa milki ya simu husika.
2. Kuhimiza utii wa sheria: Kifungu cha 128 cha EPOCA kinamtaka mtumiaji wa simu kutoa taarifa ya kupotea au kuibiwa kwa simu au laini ya simu. Kifungu cha 134 kinayataka makampuni ya simu kutokutoa huduma kwa simu ambayo imefungiwa kama ilivyoelezwa hapo juu. Mara tu mteja anapopoteza simu yake ya kiganjani anatakiwa kutoa taarifa kwa kituo cha Polisi cha karibu ambapo atapewa namba ya kumbukumbu ya taarifa ya tukio, maarufu kama RB.
Anatakiwa aende kwa mtoa huduma kutoa taarifa ya tukio akiwa na hiyo RB na uthibitisho wa umilki wa simu iliyopotea ( risiti aliyopewa wakati wa kununua iwapo itakuwepo). Mtoa huduma kwanza atahakiki umilki wa simu iliyopotea au kuibiwa na atampatia mteja namba ya kumbukumbu kwamba simu hiyo imefungiwa isutumike kwenye mitandao ya simu na hatimaye ataifungia simu hiyo ndani ya saa 24.
3. Kujenga misingi ya matumizi ya simu halisi, zisizo bandia. Mtumiaji ataweza kutambua iwapo simu aliyo nayo inakidhi viwango, ni halisi na sio bandia.
tungependa kusikia kutoka kwako, tuandikia maoni yako hapo chini.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website hii
Pia waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini

INSTAGRAM           FACEBOOK    GOOGLE+    

PINTEREST   TWITTER    LINKEDIN     DRIBBBLE

Karibu sana


LINK CLASSIC

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply