sponsor

Slider

EMBROIDERY, DTF, & SCREEN PRINTING - T-shirt, Overall, Shirt , Pylon, Kofia Nk..


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » ASKARI AFUKUZWA KAZI KWA KUTOROSHA MTUHUMIWA HUKO SIMIYU


JESHI  la polisi Mkoani Simiyu limemfukuza askari wake namba EX F3817 PC BENJAMINI kwa kosa la kumtorosha mtuhumiwa wa kesi ya mauaji aliyejulikana kwa jina la Kwandu Maduhu (70).


Tukio hilo lilitokea tarehe 27/02/2016 majira saa 1:45 jioni katika kituo cha polisi Lugulu wilaya ya Itilima Mkoani hapa, ambapo askari huyo alikuwa akifanyia kazi.


Kamanda wa polisi Mkoani hapa Onesmo Lyanga akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jana, alisema kuwa mtuhumiwa aliyetoroshwa na askari huyo alikuwa akikabiliwa na kesi ya mauaji namba ITL/IR/95/2016 ambaye ni Mkulima wa kijiji cha Gambasingu.

Lyanga alisema kuwa askari huyo amefukuzwa kazi kwa fedheha, ambapo mbali na hatu hizo atafikishwa mahakamani kwa makosa ya jinai.

Aidha Kamanda Lyanga alisema kuwa mbali na askari huyo kuchukuliwa hatua hizo, jeshi hilo linawashikilia jumla ya watu wanne kwa kuhusika na utoroshwaji wa mtuhumiwa huyo.

Aliwataja watu hao kuwa ni Juma Zakaria (40) mkazi wa kijiji cha Budalabujiga, Agnes Nzige (40) mkazi wa kijiji cha Gambasingu, Malika Kilindila (16) mkazi wa kijiji cha Gambasingu, pamoja na Robert Mandagani (62) ambaye ni mkazi wa kijiji cha Inalo.

Katika hatua nyingine Kamanda huyo alisema kuwa amefanya mabadiliko katika kikosi cha askari wa usalama barabarani, kwa kuwaondoka askari nane (8) kutokana na kukiuka maadili ya jeshi hilo.

Lyanga hakuweza kuwataja askari hao, ambapo alieleza uchunguzi dhidi yao unaendelea huku wakiwa wamehamishiwa katika vitengo vingine vya jeshi hilo.

LINK CLASSIC: Asante sana kwa kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website hii
Pia waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini

INSTAGRAM           FACEBOOK    GOOGLE +    PINTEREST   TWITTER       

LINKEDIN     DRIBBBLE    NOTJUSTOK



Karibu sana


LINK CLASSIC

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply