Mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu.
BAADA ya kipigo cha penalti 5-4 dhidi ya URA, juzi mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu Migomba ameomba radhi kwa mashabiki wa timu hiyo kutokana na matokeo mabaya.
Yanga iliondolewa kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi katika hatua ya nusu fainali na URA ya Uganda kutinga fainali dhidi ya Azam FC.
Mshambuliaji huyo alisema hawakupenda kupata matokeo ya aina ile lakini ilitokea vile kwa sababu mpira una matokeo matatu.
“Naomba mashabiki wetu wa Yanga watusamehe kwa matokeo mabaya hakuna timu ambayo inapenda kupoteza zaidi mtupe sapoti ,”alisema Ajibu.
Hata hivyo katika mchezo huo wachezaji ambao walipiga penalti ni Papy Tshishimbi, Hassan Kessy, Gadiel Michael, Daud Raphael na Obrey Chirwa ambaye alikosa.
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: