HATIMAYE Liverpool wamekamilisha mchakato wa kumsajili Virgil van Dijk kutoka Southampton kwa ada ambayo imeweka rekodi.
Ada ya usajili ya mchezaji huyo imetajwa kuwa ni pauni milioni 75, (Sh bilioni 160) ukiwa ni usajili ghali zaidi kwa upande wa walinzi.

“Nimejiunga kwenye timu kubwa duniani, Liverpool ni timu yenye heshima kubwa sana. Nilikuwa kwenye wakati mgumu kwa siku za hivi karibuni nikiwa Southampton lakini naamini kuwa sasa nitakuwa sawa.
“Ninafuraha mimi na familia yangu kuona nimekamilisha tukio hili bora kwangu. Hakika nasubiri kwa hamu kuvaa jezi nyekundu ya Liverpool kwa mara ya kwanza mbele ya mashabiki,” alisema beki huyo.
Beki huyo amesaini mkataba ambao utamweka kwenye timu hiyo hadi mwaka 2023 na mshahara wa pauni 180,000 (Sh 536m) kwa wiki.
KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA




No comments: