mtayarishaji na muongozaji wa filamu nchini aliyejipatia umaarufu kupitia filamu za OXYGEN ,AREA 51, THE HARD WAY nk ametoa ushauri kwa wasanii wenzie wa BONGO MOVIES kuacha kutafuta kiki na kutafutana uchawi kwamba nani kaua tasnia ama nani kachangia kudorora kwa sanaa ya maigizo nchini ,na kujitathmini wapi wamekosea na wapi walipatia na kuboresha upya ili kukonga nyoyo za mashabili waliopoteza imani na kazi zao
akiongea na LINK CLASSIC sydney alisema ,unajua kaka sisi tunaongea sana ilhali ukiangalia teknolojia imekua ,nasi tunatakiwa kukua nayo kwa kufanya kazi nzuri zenye viwango ,kiukweli ,mimi pia ni mmoja wa waliokuwa wakibanwa na mfumo wa ufanyaji kazi uliokuwa ukifanyika kibongobongo siwezi sema sana ila wadau wa sanaa wanajua nini namaanisha ,so sio poa kulaumu hili au lile ,mashabiki wetu wanahitaji kuona kazi nzuri sio malalamiko yetu, tizama mfano bongo flava kipindi wanauza albamu kwa mdosi ,na kisha soko lao kugoma walijitathimini kisha wakaanza mfumo mpya ngoma moja kali ,video kali promotion kubwa matokeo yake tunawaona kina kiba na kina Diamond walipo leo so nasi tukijitathmini na kujipanga upya si ujinga ni mtazamo wangu tu ila sio sheria au sio mimi ndio bora sana kuliko wenzangu , alimaliza hivyo
KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: