sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » NAIBU WAZIRI WA MALIASILI AAGIZA TFS KUANZA MCHAKATO WA KUUNDA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA MISITU

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ameiagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ianze mchakato wa kuandaa sheria ya kutoka Wakala kuwa Mamlaka ya Usimamizi wa Misitu Tanzania ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwa vile ikiendelea kubaki kuwa Wakala kuna baadhi ya mambo itashindwa kuyashughulikia.
Wakala ni Idara za Serikali zilizoondolewa kwenye serikali kuu na zina nusu mamlaka na hazina mamlaka kamili ya kujiamulia mambo yake zenyewe.Amesema uanzishwaji wa Mamlaka hiyo itasaidia kupunguza migongano kati ya misitu iliyo chini ya Tamisemi pamoja na vijiji kwa vile kutakuwa na Mamlaka moja ya kusimamia misitu tofauti na ilivyo sasa.
Ameyasema hayo jana wakati akizungumza na Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzani (TFS) makao makuu jijini Dar es Salaam.Amesema TFS kwa hatua iliyofikia kwa sasa haistahili kuwa Wakala kutokana na kazi kubwa iliyonayo hivyo inahitaji kuwa Mamlaka ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa uhuru zaidi.
Wakati akizungumza na Watumishi, Naibu Waziri Hasunga amemtaka Mtendaji Mkuu wa TFS, Dos Santos Silayo ahakikishe katika mpango mkakati utakaoandaliwa hivi sasa suala la uanzishwaji wa Mamlaka lipewe kipaumbele.Katika hatua nyingine, ameiagiza TFS iunde chombo cha kusimamia na kudhibiti ubora wa mazao ya misitu.
Amesema chombo hicho kitakuwa kikipanga mazao ya misitu kulingana na ubora wake na sio kama sasa inavyofanyika mbao zozote zile zimekuwa zikiuzwa sokoni pasipo kujali ubora wake. Amesema kuna changamoto ya bei za mbao sokoni na pia kuna changamoto ya ubora wa mbao zilizoko sokoni, Mbao nyingi zimetengenezwa kwa miti ambayo imevunwa ikiwa na miaka sita au kumi ni lazima ubora wake uwe hafifu.


KWA HABARI ZAIDI

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply