Timu ya Tanzania Bara kwa mchezo wa Beach Soka imefungwa mabao 7-6 na Malawi katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye Ufukwe wa Coco jijini Dar as Salaam.
Soka likiendelea.
Katika mchezo huo wa mashindano ya Copa Dar es Salaam, Tanzania ilicheza vizuri kipindi cha kwanza na cha pili ambapo ilimaliza ikiwa sare kwa mabao 5-5.
Piga nikupige.
Kipindi cha tatu ambacho kilikuwa cha mwisho, Malawi ikafunga mabao mawili na Tanzania moja ambapo matokeo ya mwisho yakawa Malawi 7-6 dhidi ya Tanzania.
Ngoma inogile.
Michuano hiyo inazishirikisha timu nne ambazo ni Tanzania Bara, Zanzibar, Malawi na Uganda.
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA







No comments: