Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limeeleza kuwa katika sikukuu ya Christmas na sikukuu ya kufungua zawadi(Boxing day) jumla ya mabasi ya abiri 650 yaliondoka kituo cha mabasi Ubungo na hakuna lililopata ajali.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortonatus Musilimu akizungumza na wana habari alisema kuwa ajali zilikuwa tayari zikiwapa hofu wananchi hivyo wananchi waone kipindi cha mwisho wa mwaka kama ni kipindi kingine.
“Katika kipindi cha kuanzia mwanzoni na mwishoni mwa mwaka vyanzo vikuu vya ajali imekuwa ni mwendokasi na hili tumepambana nalo kuwa nguvu kubwa kwa kusimamia tochi huko barabarani na kumekuwa na tatizo la madereva kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhali kwa maana kwamba ana over take bila kuwa makini hili sasa hivi tunapambana nalo tunapiga tochi baadae ina tumwa kwa Watsapp,” alisema Kamanda Fortonatus.
“Katika kupunguza ajali kama nilivyosema ambazo zilikuwa tayari zimeanza kuwajenga wananchi hofu, wengi walikuwa wanaogopa kusafiri na mabasi lakini katika sikukuu ya Christmas na sikukuu hii ya kufungua zawadi hasa kwa mfano tarehe 24 mwezi wa 12 mwaka 2017 yaliondoka jumla ya mabasi ya abiri 650 kutoka kituo cha mabasi Ubungo kwenda mikoa mbalimbali na katika mabasi hayo 650 hakuna basi ambalo lilipata ajali yote yalifika salama.”
KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: